Menu

Zaburi 124

ONMM

1 Kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa: 2 kama Mwenyezi Mungu hangekuwa upande wetu, watu walipotushambulia, 3 hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangetumeza tukiwa hai, 4 mafuriko yangegharikisha, maji mengi yangetufunika, 5 maji yaendayo kasi yangetuchukua. 6 Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao. 7 Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tumeokoka. 8 Msaada wetu ni katika jina la Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate