Menu

Zaburi 125

ONMM

1 Wale wamtumainio Mwenyezi Mungu ni kama Mlima Sayuni, ambao hauwezi kutikisika, bali wadumu milele. 2 Kama milima inavyozunguka Yerusalemu, ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowazunguka watu wake sasa na hata milele. 3 Fimbo ya waovu haitadumu juu ya nchi waliyopewa wenye haki, ili wenye haki wasije wakatumia mikono yao kutenda ubaya. 4 Ee Mwenyezi Mungu, watendee mema walio wema, wale walio wanyofu wa moyo. 5 Bali wale wanaogeukia njia zilizopotoka, Mwenyezi Mungu atawafukuza pamoja na watenda maovu. Amani iwe juu ya Israeli.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate