Menu

Zaburi 123

ONMM

1 Ninayainua macho yangu kwako, kwako wewe unayeketi mbinguni kwenye kiti chako cha enzi. 2 Kama vile macho ya watumwa yatazamavyo mkono wa bwana wao, kama vile macho ya mjakazi yatazamavyo mkono wa bibi yake, ndivyo macho yetu yamtazamavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hadi atakapotuhurumia. 3 Uturehemu, Ee Mwenyezi Mungu, uturehemu, kwa maana tumevumilia dharau nyingi. 4 Tumevumilia dhihaka nyingi kutoka kwa wenye kiburi, dharau nyingi kutoka kwa wenye majivuno.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate