Menu

Zaburi 122

ONMM

1 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani mwa Mwenyezi Mungu." 2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako. 3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ulioshikamana pamoja. 4 Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Mwenyezi Mungu, kulisifu jina la Mwenyezi Mungu kulingana na maagizo waliopewa Israeli. 5 Huko viti vya hukumu hukaa, viti vya ufalme vya nyumba ya Daudi. 6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wanaokupenda na wawe salama. 7 Amani na iwe ndani ya kuta zako, na usalama ndani ya ngome zako." 8 Kwa ajili ya ndugu na rafiki zangu, nitasema, “Amani iwe ndani yako." 9 Kwa ajili ya nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate