Menu

Zaburi 121

ONMM

1 Nayainua macho yangu natazama milima: msaada wangu utatoka wapi? 2 Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia. 3 Hatauacha mguu wako uteleze, yeye akulindaye hatasinzia, 4 hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi. 5 Mwenyezi Mungu anakulinda, Mwenyezi Mungu ni uvuli wako mkono wako wa kuume, 6 jua halitakudhuru mchana, wala mwezi wakati wa usiku. 7 Mwenyezi Mungu atakukinga na madhara yote, atayalinda maisha yako, 8 Mwenyezi Mungu atakulinda unapoingia na unapotoka, tangu sasa na hata milele.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate