Menu

Zaburi 125

ULB

1 Wale wamwaminio Yahwe ni kama mlima Sayuni, hautikisiki, wadumu milele. 2 Kama milima inavyo izunguka Yerusalemu, hivyo ndivyo Yahwe anavyo wazunguka watu wake sasa na hata milele. 3 Fimbo ya uovu haitatawala katika nchi ya wenye haki. Vinginevyo wenye haki wanaweza kukosea. 4 Ee Yahwe, utende wema kwa wale walio wema na wale walio wanyoofu mioyoni mwao. 5 Lakini kwa wale wanaogeukia njia zao za upotovu, Yahwe atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate