Menu

Zaburi 93

ONMM

1 Mwenyezi Mungu anatawala, amejivika utukufu; Mwenyezi Mungu amejivika utukufu tena amejivika nguvu. Dunia imewekwa imara, haitaondoshwa. 2 Kiti chako cha enzi kimekuwa thabiti tangu zamani; wewe umekuwa tangu milele. 3 Bahari zimepaza, Ee Mwenyezi Mungu, bahari zimepaza sauti zake; bahari zimepaza sauti za mawimbi yake. 4 Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Mwenyezi Mungu aishiye juu sana ni mkuu. 5 Ee Mwenyezi Mungu, sheria zako ni imara; utakatifu umepamba nyumba yako pasipo mwisho.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate