Menu

Zaburi 70

ONMM

1 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa; Ee Mwenyezi Mungu, njoo hima unisaidie. 2 Wale wanaotafuta kuniua, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu. 3 Wale wanaoniambia, “Aha! Aha!” na warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao. 4 Lakini wote wanaokutafuta washangilie na kukufurahia, wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme, “Mwenyezi Mungu ni mkuu!" 5 Lakini mimi bado ni maskini na mhitaji; Ee Mungu, unijie haraka. Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu; Ee Mwenyezi Mungu, usikawie.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate