Menu

Zaburi 61

ONMM

1 Ee Mungu, sikia kilio changu, usikilize maombi yangu. 2 Kutoka miisho ya dunia ninakuita, ninakuita huku moyo wangu unadhoofika; uniongoze kwenye mwamba ulio juu kuniliko. 3 Kwa kuwa umekuwa kimbilio langu, ngome imara dhidi ya adui. 4 Natamani kukaa kwenye hema lako milele, na kukimbilia chini ya uvuli wa mabawa yako. 5 Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako. 6 Mwongezee mfalme siku za maisha yake, miaka yake kwa vizazi vingi. 7 Mtawaze mbele za Mungu milele; amuru upendo wako na uaminifu wako vimlinde. 8 Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate