Menu

Zaburi 134

ONMM

1 Msifuni Mwenyezi Mungu, ninyi nyote watumishi wa Mwenyezi Mungu, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Mwenyezi Mungu. 2 Inueni mikono yenu katika patakatifu na kumsifu Mwenyezi Mungu. 3 Naye Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate