Menu

Zaburi 129

ONMM

1 Wamenitesa sana tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: 2 wamenitesa sana tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. 3 Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu. 4 Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. 5 Wale wote wanaoichukia Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. 6 Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; 7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake. 8 Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu."

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate