Menu

Zaburi 127

ONMM

1 Mwenyezi Mungu asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Mwenyezi Mungu asipoulinda mji, walinzi wakesha bure. 2 Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapendwa wake. 3 Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu, uzao ni zawadi kutoka kwake. 4 Kama mishale mikononi mwa shujaa ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake. 5 Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate