Menu

Zaburi 113

ONMM

1 Msifuni Mwenyezi Mungu. Enyi watumishi wa Mwenyezi Mungu msifuni, lisifuni jina la Mwenyezi Mungu. 2 Jina la Mwenyezi Mungu na lisifiwe, sasa na hata milele. 3 Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake, jina la Mwenyezi Mungu linapaswa kusifiwa. 4 Mwenyezi Mungu ametukuka juu ya mataifa yote, utukufu wake juu ya mbingu. 5 Ni nani aliye kama Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, Yule aliyeketi kwenye kiti cha enzi huko juu, 6 ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi? 7 Huwainua maskini kutoka mavumbini, na kuwanyanyua wahitaji kutoka lundo la majivu, 8 huwaketisha pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. 9 Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake, akiwa mama watoto mwenye furaha. Msifuni Mwenyezi Mungu.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate