Menu

Zaburi 110

ONMM

1 Mwenyezi Mungu amwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya adui zako kuwa mahali pa kuweka miguu yako." 2 Mwenyezi Mungu ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni; utatawala katikati ya adui zako. 3 Askari wako watajitolea kwa hiari katika siku yako ya vita. Ukiwa umevikwa fahari takatifu, kutoka tumbo la mapambazuko utapokea umande wa ujana wako . 4 Mwenyezi Mungu ameapa, naye hatabadilisha mawazo yake: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki." 5 Bwana yuko mkono wako wa kuume, atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake. 6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga na kuwaponda watawala wa dunia nzima. 7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia ; kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate