Menu

Zaburi 100

ONMM

1 Mpigieni Mwenyezi Mungu kelele za shangwe, dunia yote. 2 Mwabuduni Mwenyezi Mungu kwa furaha; njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe. 3 Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu. Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake; sisi tu watu wake, kondoo wa malisho yake. 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na katika nyua zake kwa kusifu, mshukuruni yeye na kulisifu jina lake. 5 Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema na fadhili zake zadumu milele; uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate