Menu

Zaburi 54

BIB

1 Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako. 2 Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu. 3 Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu. 4 Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza. 5 Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize. 6 Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema. 7 Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate