Menu

Zaburi 131

BIB

1 Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu. 2 Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu. 3 Ee Israeli, mtumaini Bwana tangu sasa na hata milele.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate