Menu

Zaburi 129

BIB

1 Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: 2 wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. 3 Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu. 4 Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. 5 Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. 6 Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; 7 kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake. 8 Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana."

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate