Menu

Zaburi 124

BIB

1 Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa: 2 kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia, 3 wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai, 4 mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika, 5 maji yaendayo kasi yangalituchukua. 6 Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao. 7 Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka. 8 Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate