Menu

Zaburi 122

BIB

1 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia, “Twende nyumbani ya Bwana." 2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama malangoni mwako. 3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji ambao umeshikamanishwa pamoja. 4 Huko ndiko makabila hukwea, makabila ya Bwana, kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo waliopewa Israeli. 5 Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. 6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu: “Wote wakupendao na wawe salama. 7 Amani na iwepo ndani ya kuta zako na usalama ndani ya ngome zako." 8 Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki, nitasema, “Amani iwe ndani yako." 9 Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nitatafuta mafanikio yako.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate