Menu

Ezra 2

BIB

1 Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 2 wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa: 3 wazao wa Paroshi2,172 4 wazao wa Shefatia372 5 wazao wa Ara775 6 wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu)2,812 7 wazao wa Elamu1,254 8 wazao wa Zatu945 9 wazao wa Zakai760 10 wazao wa Bani642 11 wazao wa Bebai623 12 wazao wa Azgadi1,222 13 wazao wa Adonikamu666 14 wazao wa Bigwai2,056 15 wazao wa Adini454 16 wazao wa Ateri (kupitia Hezekia)98 17 wazao wa Besai323 18 wazao wa Yora112 19 wazao wa Hashumu223 20 wazao wa Gibari95 21 watu wa Bethlehemu123 22 watu wa Netofa56 23 watu wa Anathothi128 24 watu wa Azmawethi42 25 wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi743 26 wazao wa Rama na Geba621 27 watu wa Mikmashi122 28 watu wa Betheli na Ai223 29 wazao wa Nebo52 30 wazao wa Magbishi156 31 wazao wa Elamu ile ingine1,254 32 wazao wa Harimu320 33 wazao wa Lodi, Hadidi na Ono725 34 wazao wa Yeriko345 35 wazao wa Senaa3,630 36 Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua)973 37 wazao wa Imeri1,052 38 wazao wa Pashuri1,247 39 wazao wa Harimu1,017 40 Walawi: wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia)74 41 Waimbaji: wazao wa Asafu128 42 Mabawabu wa lango la Hekalu: wazao waShalumu, Ateri, Talmoni,Akubu, Hatita na Shobai139 43 Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, 44 wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni, 45 wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu, 46 wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani, 47 wazao wa Gideli, Gahari, Reaya, 48 wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu, 49 wazao wa Uza, Pasea, Besai, 50 wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu, 51 wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri, 52 wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha, 53 wazao wa Barkosi, Sisera, Tema, 54 wazao wa Nesia na Hatifa. 55 Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda, 56 wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli, 57 wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami. 58 Watumishi wa Hekalu wote nawazao wa watumishiwa Solomoni392 59 Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli: 60 wazao waDelaya, Tobia na Nekoda652 61 Kutoka miongoni mwa makuhani: Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). 62 Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 63 Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu. 64 Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 65 tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. 66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, 67 ngamia 435 na punda 6,720. 68 Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 69 Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo. 70 Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao.

Everything we make is available for free because of a generous community of supporters.

Donate